
Timu ya taifa ya Brazil alfajiri ya leo imekuwa ni timu ya kwanza kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 Russia, baada ya kuifunga timu ya taifa ya Paraguay kwa magoli 3-0.

Magoli ya Brazil yalifungwa na Coutinho alifunga goli la kwanza na la
pili lilifungwa na Neymar na goli la mwisho lilikuwa katika dakika tano
za mwisho ambapo Coutinho alicheza vyema kwa muuganiko na Marcelo, ambao
walipeleka pasi kwa Paulinho aliyekuwa amepanda mbele na akauunganisha
mpira kwa kisigino ukakuta Marcelo aliyekuwa anakimbia na kufunga kwa
urahisi.
Brazil katika kundi lake yupo na timua za Uruguay, Peru na Paraguay.

No comments:
Post a Comment