Mkuu wa wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi amepiga marufuku shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo la hifadhi la ranchi ya NARCO na kuwaagiza viongozi wa vijiji kurudisha kwa wananchi ardhi yote iliyouzwa kinyume na sheria ya ardhi.
Ndejembi ametoa amri hiyo baada ya wakazi wanaozunguka eneo la ranchi ya NARCO kuvamia hifadhi hiyo na kufanya shughuli za kilimo na mifugo.
Pia Ndejembi awataka viongzi na wananchi kukaa na kupanga upya matumizi ya ardhi kisheria baada ya kusikiliza malalamiko na sababu za wananchi kuvamia hifadhi.

No comments:
Post a Comment