Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Ezekiel Odunga akizungumza na wananchi wa kata ya Farkwa wakati wa uzinduzi wa zoezi la uthamini mali ili kupisha ujenzi wa bwawa la Farkwa.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma akiongozana na baadhi wa
Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Chemba, Wataalamu wa Halmashauri, Wataalamu kutoka Wizara ya
Maji, Uvuvi na umwaguliaji, Wataalamu wa Bonde la Kati na Wataalamu
kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wamezindua zoezi la uthamini wa mali za
wananchi wa vijiji viwili vya Mombose na Bubutole watakaohama kupisha
mradi mkubwa wa Ujenzi wa bwawa la Farkwa mkoani hapa.
Mradi wa bwawa la Farkwa ni mradi mkubwa ambao huenda ukawa ni
mkubwa katika Ujenzi wa mabwawa makubwa kuliko yote barani Afrika. Mradi
huu uliasisiwa na baba wa Taifa tangu mwaka 1970 utazinufaisha Wilaya
za Bahi, Chemba, Chamwino na Dodoma Manispaa na utegemea kutumia pesa za
Tanzania zaidi ya Tilioni 2.
Kufuatia umuhimu wa mradi huu na uwijio wa makao makuu ya nchi
mkoani Dodoma, serikali imezamilia ifikapo mei mwaka huu zoezi la
Uthamini wa mali za wananchi wanaohama kupisha mradi huu mkubwa katika
Vijijini vya Mombose na Bubutole vilivyopo Wilayani Chemba pamoja na
vijiji vinavyopitiwa na njia Kuu ya bomba linalopeleka Maji eneo la
Kilimani mjini Dodoma liwe limekamilika tayari kwa kuwalipa wananchi ili
Ujenzi wa bwawa uanze.
Ujenzi wa mradi huu unategemea kuchukua miaka mitatu 2017-2021
mpaka kukamilika kwake. Hivyo wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa
Wataalamu wa uthamini kwa kuwa wameusubiri mradi huu kwa zaidi ya miaka
47 na leo serikali imepata fedha ya kuutekeleza.
Mhe Mkuu wa Wilaya ya Chemba Ndugu Simon Odunga wamewataka wananchi
hao kujiepusha na watu wasiopenda maendeleo yao na nchi yetu kwa ujumla
wa anaopita pita huko na kujifanya watetezi wa haki za wananchi. Swali
hao watetezi walikuwa wapi tangu 1970 waje leo ambapo mradi unaanza
kutekelezwa.?
Aidha, amesisitiza wananchi ambao ni wamiliki halali wa maeneo
husika ndio wajitokeze kwenye uthamini huo ili kuepusha udanganyifu na
migogoro isiyo ya lazima wakati wa malipo yatakopoanza. Kwani kuna
baadhi ya wananchi ni waaminifu na atakayefanya hivyo akibaini sheria
kali dhidi yake zitachukua mkondo.
Kwa upande wa Wataalamu Mkuu huyo wa Wilaya amewataka kutumia
akili, uweledi na taaluma zao katika kuhakikisha kila mwananchi wa
maeneo hayo anapata haki yake stahiki kwa mujibu wa sheria za uthamini.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba,
Mhe Rajabu Muheshimwa ameongea kwa kupongeza juhudi za Serikali kwa
kuamua kuanza mradi huu na zaidi kusihi wananchi kutoa ushirikiano kwa
Wataalamu, hali kadhalika Mhe Diwani wa Kata ya Farkwa Ndugu, Suleiman
Gawa amesisitiza kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu pia
Wataalamu wahakikishe wanaorodhesha mali zote za wananchi
zinazotambulika kisheria ili kuepusha migongano hapo baadae.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya amewataka Viongozi wa Vijiji na
vitongoji kusimamia zoezi hili kikamilifu kwani wao ndio wanaowafahamu
wananchi wao pia watoto ambao wanamiliki mali lakini hawatambuliwi
kisheria kutokana na umri wao.

No comments:
Post a Comment