
Rubani ndege aina ya Boeng 737-800,
William “Mike” Grubbs amefariki huku ndege hiyo ikiwa safarini kutoka
Dallas kwenda Albuquerque huko New Mexico, kwa mujibu wa shirika la
American Airlines.
Ndege hiyo ilikuwa imesalia na karibu kilomita tatu kabla ya kutua, wakati nahodha alitangaza dharura, kwa mujibu wa msemaji wa uwanja wa ndege wa Albuquerque
Ndege hiyo ilitua salama bila hatari yoyote kutokea uwajani na hakuna rubani yoyoye aliyejeruhiwa.
Tukio jengine kama hilo limetokea Mwaka 2015 ambapo rubani mwingine wa shirika hilo alifariki wakati wa safari kutoka Phoenix kuelekea Boston.
Ndege hiyo ilipelekwa na rubani mweza kwa njia iliyo salama hadi uwanja wa Syracuse mjini New York

No comments:
Post a Comment