KATIBU Tawala wa wilaya ya Hanang,Mkoani
Manyara Bi Sara Sanga amekemea tabia ya kupotosha tiba na chanjo kwa
kuzihusisha na imani za kishirikina.
Katibu Tawala huyo ameyasema hayo kwenye
maadhimisho ya wiki ya chanjo duniani iliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha
Gitting, wilayani Hanang, Mkoani Manyara.
Akizungumzia kuhusu hali ya chanjo katika
wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2015 hadi 2017,Bi Sanga amesema kuwa kati ya
lengo la kuchanja watoto elfu 65 na 408 kila mwaka lililowekwa na wilaya
hiyo,kwa mwaka 2015 wilaya hiyo ilivuka lengo kwa kuchanja watoto 66 elfu na 7 na 16 sawa na asilimia 102.

No comments:
Post a Comment