LATEST NEWS

Friday, May 12, 2017

Majeruhi watatu katika ajali ya gari iliyotokea wilayani karatu wanatarajiwa kusafirishwa siku ya kesho

Majeruhi watatu katika ajali ya gari iliyotokea wilayani karatu wanatarajiwa kusafirishwa siku ya tarehe 13 mwezi wa tano kwa ndege maalumu kupelekwa nchini marekani kwa matibabu.

Akizungumza na wandishi wa habari mganga mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Arusha Mount meru dr Jacklin Urio ameeleza kuwa kwa sasa watoto hao wanaendelea vizuri ambapo kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za kuwasafirisha kwenda nchini marekani kwa matibabu.

Licha ya mganga mfawidhi kuzungumzia hayo kwa upande Wake mganga mkuu wa hospital ya mkoa naye akaweza kubainisha juu ya kusafirishwa kwa watoto hao Pamoja na hali zao.


Mbunge wa Jimbo la Singida kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye pia ameshiriki hatua zote za kuhakikisha watoto hao wanapata matibabu akazungumzia wahisani waliojitolea kutoa ndege kuwapeleka watoto hao.

Watoto hao watatu ambao ni majeruhi walinusurika katika ajali ya gari iliyotokea wilayani karatu mnamo tarehe tano mwezi may mwaka huu na kusababisha vifo vya wenzao 35 wanaendelea vizuri​huku pia watanzania wakitakiwa kuzidi kufanya maombi kwa watoto hao.

No comments:

Post a Comment

Adbox