LATEST NEWS

Tuesday, May 16, 2017

Mti ulie machozi ya damu!..NO, Hapana - TANROADS



 

Taarifa ya kuwapo kwa mti uliodaiwa kuliamachozi ya damu wakati ukikatwa zimekanushwa na Meneja wa Tanroad mkoani mwanza.

Meneja huyo wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Marwa Rubirya amesema habari za mti huo si za kweli na kuwa mti huo umeshakatwa.

"Huu ulikuwa uzushi hakuna kitu kama hicho sema kilichotokea ni kwamba mashine iliyopelekwa awali ilikuwa haina nguvu ikilinganishwa na ugumu wa mti huo,"amesema Rubirya. Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kuzusha mambo ambayo hayana ukweli na kuibua hisia zisizo na msingi wowote.

No comments:

Post a Comment

Adbox