Na Anna Mchome ; Arusha
Kesi ya kughushi nyaraka na
kujifanya Afisa usalama wa Taifa,inayomkabili mwenyekiti wa uvccm mkoa
wa Arusha,Lengai Ole Sabaya imeshindwa kuendelea Mara baada ya upande wa
Mashtaka kudai haina nia ya kuendelea na shauri hilo.
Akizungumza
mahakamani hapo mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga,Wakili wa serikali
Grace Madikenya alisema kuwa jamhuri kupitia kifungu namba 91 cha
mwenendo wa makosa ya jinai haina nia na shauri hilo kutokana na shahidi
wake muhimu kwenda masomoni nje ya nchi.
"Mheshimiwa
hakimu upande wa jamhuri haina nia ya kuendelea na shauri hilo chini ya
kifungu namba 91 cha mwenendo wa makosa ya jinai"Alisema wakili wa
serikali
Hata hivyo
Wakili wa upande wa mshitakiwa,Grace Mndeme na Charles Abrahamu
waliweka pingamizi juu ya hoja hiyo walidai kuwa Wakili wa serikali
wanania ya kuichezea mahakama na wanalengo la kumtesa mteja wao.
"
Mheshimiwa sisi tunapinga hoja iliyoletwa mbele yako na Wakili msomi wa
serikali kwa sababu upande wa jamhuri wanaitumia vibaya mahakama na
wanania ya kumtesa mshitakiwa,na si Mara yao ya kwanza kufanya
hivyo"Alisema Mndeme
Alieleza
kuwa hoja ya wakili wa serikali haina nia njema na mshitakiwa kwani sio
Mara ya kwanza kueleza nia ya kutoendelea na shauri hilo na baadae
mtuhumiwa anapoachiwa hukamatwa na kulazwa mahabusu na baadae
kufikishwa mahakama na kushitakiwa kwa shauri hilo hilo.
Pia
aliieleza mahakama hiyo kuwa kumekuwepo na uzembe katika uendeshaji wa
shauri hilo unaofanywa na Mwanasheria wa serikali ,kwa sababu wakati
kesi hiyo inaendelea walishindwa kuleta mashahidi badala yake
walikimbilia kuliondoa shauri hilo mahakamani.
Baada
ya kuwepo kwa pingamizi hilo kutoka kwa mawakili wa mshitakiwa ,hakimu
Mwankuga aliahirisha shauri hilo kwa Madai kuwa atatoa uamuzi Mdogo siku
ya Ijumaa ,Mai 28 mwaka huu.
Akizungumza
nje ya mahakama mshitakiwa, Sabaya alieleza kukerwa na hatua ya upande
wa serikali kuendelea kupiga danadana kesi yake alidai kuwa kuna mpango
wa kuendelea kumdhalilisha kwani yeye ni mwanasiasa aliyechaguliwa na
wananchi anahitaji kuwatumikia .
No comments:
Post a Comment