
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama askari wanaume katika maeneo yao ya kazi.
Amesisitiza kuwa muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.
“Vyeo haviji tu ni lazima polisi wanawake muonyeshe kuwa mnaweza ili muweze kupandishwa vyeo na kupata nafasi za uongozi katika Majeshi yenu”
Kuhusu utendaji kazi wa Polisi wanawake, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku Tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.
Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema anaimani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.
Masauni pia amewahimiza polisi wanawake wanaopata mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha na wenzao mipango na mikakati waliyoweka katika kulinda raia na mali zao katika nchi zao.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano huo
mapema leo Mei 17.2017 Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ukiendelea

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akibadilishana mawazo na
baadhi ya Polisi Wanawake wakati wa tukio hilo la ufunguzi

Polisi Wanawake wakiwa katika
tukio hilo la ufunzi wa mkutano maalum wa siku tatu ambao umefunguliwa
na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu.
No comments:
Post a Comment