![]() |
Rais Trump ameongeza makubaliano ya mpango wa kinyuklia kati ya Marekani na Iran |
Ikulu ya Whitehouse
nchini Marekani imeendeleza mpango wa kuipunguzia vikwazo Iran licha ya
rais Donald Trump kuukosa mpango huo.
Bwana Trump ameelezea makubaliano hayo kuwa mabaya zaidi.
Hatahivyo wizara ya fedha nchini humo iliwawekea vikwazo maafisa fulani na mfanyibiashara wa China anayehusishwa na mpango wa makombora wa Iran.
Hatua hiyo inamaanisha vikwazo vinavyozuia kampuni zozote za Marekani zinazoiuzia ama kushirikiana na Iran vitaendelea kulemazwa.
Kwa upande wake Iran imekubali kupunguza mipango yake ya nyuklia, kupunguza uhifadhi wa madini ya Uranium, uzalishaji wa Plutonium na kuwaruhusu wachunguzi kuchunguza vifaa vyake.
Vikwazo vipya kutoka kwa wizara ya fedha vinaathiri watu binafsi wakiwemo maafisa wawili wa Iran katika idara ya ulinzi na wanaouza makombora ya kijeshi ili kulipiza kisasai jaribio la kombora pamoja na hatua ya Iran kumuunga mkono Bashar al-Assad wa Syria.
Raia wa Marekani na washirika wake sasa hawaruhusiwi kuingia mikataba na maafisa hao na kampuni husika.
No comments:
Post a Comment