LATEST NEWS

Friday, September 8, 2017

Wachezaji tisa waliomshambulia mwamuzi Nigeria wapigwa marufuku



Wachezaji tisa na maafisa wawili wa klabu wamepigwa marufuku ya mechi 12 na 19 mtawalia kwa kuwashambulia waamuzi wakati wa mechi ya ligi nchini Nigeria.

Klabu hiyo FC Ifeanyi Ubah iliingia kwenye ushirikiano rasmi na West Ham ya Uingereza mwaka jana.Wakati wa mechi hiyo Agosti, wachezaji watatu walimshambulia refarii Nakura Auwal baada ya winga King Osanga kufukuzwa uwanjani.

Wachezaji wengine sita walijiunga na mfarakano huo.

Maafisa wawili wa klabu, Chidi Nwogu na Adrika Obiefuna, pia walishiriki

Wachezaji wawili kati ya walioadhibiwa na wasimamizi wa Ligi Kuu ya Nigeria, Stephen Eze na Adeleye Olamilekan, wamewahi kuchezea timu ya taifa ya Nigeria katika mechi za Ligi ya Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani.

Klabu hiyo pia imepigwa faini ya $4,900 kwa sababu ya kisa hicho na pia ikatakiwa kulipa waamuzi walioshambuliwa $700 kila mmoja.

Aidha, klabu hiyo itatakiwa kulipia gharama ya matibabu.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za karibuni za kujaribu kukabiliana na visa vya waamuzi kushambuliwa na mashabiki kuzua fujo mechi za ligi kuu.

No comments:

Post a Comment

Adbox