LATEST NEWS

Thursday, February 9, 2017

Polisi MWANZA waagizwa kuongeza mapambano ya dawa za kulevya



Jeshi la polisi mkoani MWANZA limewaagiza maafisa mbalimbali wa jeshi hilo kuongeza mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya na kuwataka wale wanaojihusisha na biashara hiyo kuacha mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.

Agizo hilo limetolewa na Kamanda wa polisi wa mkoa wa MWANZA, – AHMED MSANGI wakati wa akikagua unadhifu wa maafisa na askari polisi.

Kamanda MSANGI pia amekemea vitendo vya rushwa miongoni mwa maafisa wa jeshi la polisi mkoani MWANZA na kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wafanye kazi kwa uadilifu.

No comments:

Post a Comment

Adbox