Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba.
Akizungumza juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama watu wenye ualbino kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza na Shinyanga na wanachama wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa Josephat Torner vitendo vya kufua makaburi ya watu wenye ualbino yanatishia amani yao
Torner alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu katika masuala ya mauaji na ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu wenye ualbino waishi kwa amani ndani ya nchi yao. “Katika suala la mauaji ya watu wenye ualbino ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu tunaomba serikali hata kuwataja kwa majina wanunuzi hao kama ilivyotokea kwenye masuala ya vita ya dawa zakulevya na uuzaji bombe aina ya viroba”,alisema Torner.
Aidha alisema wanalaani kitendo cha kufukuliwa kwa kaburi la Nelson Msogole (50) aliyekuwa akiishi mji wa Songwe baada ya kufariki tarehe 28/3/2011 na kaburi lake kuonekana kufukuliwa tarehe 20/3/2017na watu wasiojulikana. “Matukio haya yanaendeshwa kwa usiri hivyo tunahoji kwanini imeshindikana ikiwa kwenye dawa za kulevya wameweza kutaja na kumepiga hatua?”,alihoji Torner.
Picha na Suzy Butondo-Malunde1 blog.

No comments:
Post a Comment