
Mshiriki wa zamani wa Miss Tanzania, Nargis Mohamed ameingia kwenye biashara mpya ya urembo kupitia mtandao.
Akiwa na Nafue Nyange anayefahamika zaidi Kama GlamMadam wameamua
kuandaa mafunzo maalum katika fani ya urembo kwaajili ya wanawake na
vijana ambao wangependa kujifunza fani hii ya urembo.
“Mafunzo hayo hayachagui jinsia, nia yeti kubwa sisi ni kuwawezesha
wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali
na kujijenga kimaisha sambamba na mpango wa serikali yetu kujenga ajira
na kujikwamua kutoka kwenye umaskini,” alisema Nargis Mohamed.
Mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia tovuti yao
www.glammadamlive.com, na wataosajiliwa wataweza kufanya malipo kupitia
Vodacom M-pesa na Tigo Pesa. Kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kutumia
kadi tofauti kama VISA,MasterCard,American Express na Kadhalika.
Gharama ni shillingi elfu 10 tu za kitanzania kwa mwezi. Wasajili
watahitaji simu au tablet ya aina yeyote kama iPad,Samsung na kadhalika.
Tujiwezeshe na tujiinue kwa fani hii ya urembo na ujuzi huu,pamoja
watanzania tunaweza.

No comments:
Post a Comment