LATEST NEWS

Thursday, March 23, 2017

Rais afanya ziara ya kushtukiza bandarini

Rais John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam leo. Katika ziara hiyo Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini uliozuiwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi Machi 2, 2017. Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

No comments:

Post a Comment

Adbox