Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu ameagiza kuanzishwa duka la Dawa ndani ya miezi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Hayo ameyasema wakati wa ziara ya
kikazi mkoani Iringa leo tarehe ambapo ametembelea Kituo cha Damu
Salama cha Mkoa pamoja na Hospitali ya wilaya ya Mafinga
“Pia naagiza Uongozi wa Hospitali zote za Mikoa na Wilaya kuanzisha Wodi za
Watoto Wachanga na Watoto Njiti mara moja” alisema Mh. Ummy.
Mbali na hayo Waziri Ummy ameagiza kujengwa kwa Kitengo cha Wagonjwa wa
Dharura (Emergency Unit) kwa hospitali hizo mara moja ili kuboresha
huduma ya afya kwa wakazi wa Iringa.
Akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za Afya katika mkoa mbele ya Waziri wa Afya,Mh Amina Masenza,mkuu wa Mkoa wa Iringa alieleza hatua mbalimbali wanazochukua katika
kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo vya
Afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, utoaji wa elimu ya uzazi
wa mpango pamoja na lishe kwa wananchi bila kusahau kuhamasisha
wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Hata hivyo,zipo changamoto kadhaa zinazowakabili mkoa kufikia lengo la lao kutoa
huduma bora za Afya. Mathalani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya
Iringa haina wodi/kitengo cha dharura, upungufu wa watumishi, Ufinyu wa
eneo la Hospitali, ukosefu wa Gari la Kubebea Wagonjwa na ukosefu wa
baadhi ya vitendanishi.

No comments:
Post a Comment