Wachezaji wa klabu ya Chelsea, N’Golo Kante na Eden Hazard wameingia kwenye fainali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA).
Kante pia aliingia Sita Bora mwaka jana kuwania tuzo hiyo akiwa anachezea Leicester City, ambao ni mabingwa wa ligi kuu Uengereza, lakini hakufanikiwa kufika Tatu Bora, ila mwaka huu anapewa nafasi kubwa ya kushinda.
Wengine ambao wameingia katika hatua hii ni Alexis Sanchez wa Arsenal, Zlatan Ibrahimovic wa Manchester United, Romelu Lukaku wa Everton na Harry Kane wa Tottenham Hotspur.
Wakati Kane wa Tottenham akiingia hatua hiyo, mchezaji mwenzake Dele Alli hayumo licha ya chipukizi huyo wa kimataifa wa Uingereza kufanya vizuri msimu uliopita.
Mchezaji mwingine ana bahati mbaya kwa kukosekana kwenye hatua hii ni mshambuliaji wa Sunderland, Jermain Defoe ambaye licha ya kuwa na umri wa miaka 34 sasa amewafungia mabao 14 Black Cats.
Hawa ndio wachezaji ambao wanawania tuzo ya (PFA)
Alexis Sanchez (Arsenal)
Eden Hazard (Chelsea)
N’Golo Kante (Chelsea)
Romelu Lukaku (Everton)
Zlatan Ibrahimovic (Man United)
Harry Kane (Tottenham)
Thursday, April 13, 2017
Fahamu wachezaji walioingia sita bora ya tuzo za PFA England
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment