Wakimbiaji Ruth Chepng'etich wa Kenya na Ismail Juma wa Tanzania ndio washindi wa mbio za Istanbul Half Marathon mwaka 2017. Kwa upande wa akina dada, Chepng'etich ametumia saa 1:06:19, nafasi ya pili imechukuliwa na Eunice Kirwa kutoka Bahrain aliyetumia saa 1:06:46 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Muethiopia Worknesh Degefa alikamata nafasi ya tatu kwa kutumia saa 1:08:55.Kwa upande wa wanaume, Ismail Juma wa Tanzania, ametawazwa kuwa bingwa baada ya kutumia saa 1:00:09 ambayo ni rekodi mpya. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Terefa Debela kutoka Ethiopia kwa kutumia saa 1:00:22, naye Edward Rotich alishika nafasi ya tatu baada ya kutumia saa 1:00:37.
Sunday, April 30, 2017
Mkenya na Mtanzania watwaa ushindi mbio fupi Instabul
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment