Madaktari 258 ambao walikidhi vigezo vya kwenda kufanya kazi nchini Kenya, sasa wataajiriwa na serikali ya Tanzania kutokana na kuwepo na zuio la Mahakama ya Kenya la kuwaajiri.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Rais Magufuli kumwelekeza jana
kuwa awaajiri madaktari hao pamoja na wataalam wengine wa afya 11.
Madakatari hao walioomba hizo nafasi za kwenda Kenya walikuwa 496 kati ya 500 waliotakiwa, 258 ndio wakakidhi vigezo.
Mkataba
wa Tanzania na Kenya ilikuwa mpaka Aprili 6 wawe wamepatikana hao
madaktari na kati ya Aprili 6 mpaka 10 wasafirishwe kwenda Kenya, sasa
baada ya kuajiriwa na serikali, Kenya wakiwa tayari na kuhitaji tena
madaktari watatafutiwa wengine.
No comments:
Post a Comment