Katika
kuazimisha siku ya kimataifa ya msichana na Tehama,Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA kanda ya kaskazini imeiazimisha
siku hiyo na wanafunzi wa shule ya sekondari ya longido mkoani Arusha kwa
kuwahamasisha wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na technolojia ya Tehama
na kutoa elimu ya mawasiliano ili kutumia mtandao kwa njia sahihi
WANAFUNZI WA SHULE YA LONGIDO SEKONDARI WAKIWA KATIKA DARASA LA KOMPYUTA
Akizungumzia
siku hiyo ya msichana na Tehama na umuhimu
wa wanafunzi kujifunza somo hilo,maneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya
kaskazini Mhandisi Annet mahimbo matindi
amesema kuwa,soko la Tehama linauhitaji wa watu wengi sasa na lina fursa nyingi sana hasa kwa wanawake
hivyo wasichana wanatakiwa kutokuogopa
masomo hayo ili kukutana na furusa nyingi za ajira
"Tumekuja hapa kukutana na wasichana wanaosoma katika shule hii ya longido sekondari,Tumewafahamisha umuhimu na faida za TEHAMA,na pia tumewahamasisha wasiogope masomo ya sayansi kwasababu yana future nzuri"
MHANDISI ANNET MAHIMBO MATINDI AKIELEKEZWA NA WASICHANA NA SHULE YA LONGIDO JINSI WANAVYOSOMA COMPYUTA JIJINI ARUSHA
Wakizungumzia
siku hiyo ya wasichana,Baadhi ya wasichana wa shule ya longido sekondari wanasema wanashukuru mamlaka
ya mawasiliano Kanda ya kaskazini kuwatembelea na kuwafundisha mengi kuhusu
Tehama ila mbali na hayo wanachangamoto nyingi kama vitabu,walimu, vifaa vya
kutosha vya kujisomea kama za kompyuta za watu wenye walemavu wa macho
"Tunawashukuru na tunafurahi TCRA kwa kututembelea shuleni kwetu leo na kuazimisha siku hii ya msichana na TEHAMA duniani kote,tunashukuru mmekuja kuongea na sisi ili kutupa hamasa zaidi kufanya vitu kuhusuna na tehama zaidi ili kupata kipato ama kujipatia furusa mbalimbali duniani kote,kwasababu ukisoma tehama unaweza kufanya kazi popote pale nchini na duniani serikalini au sekta binafsi"
"Na mkisimama hapa kama mnavyoona hawa ndo walimu wetu wawili wa tehama,hiki ndo chumba chetu ambacho tunatumia kuhusiana na TEHAMA japokuwa tunavifaa vichache lakini kidogo vinatusaidia na bhado wenye uoni afifu wanavifaa pia vichache kama mnavyoviona hapa,na tunawashukuru sana kuja shuleni kwetu tunawakaribisha tena muendelee kututembelea na kuzidi kutuongezea hamasa na mtuongezee hata chumba kingine cha kompyuta ili viweze kututosheleza kwa idadi ya wanafunzi"
"wasichana wengi wamekuwa wakiogopa masomo ya sayansi wakikwepa kwamba wawanatumia muda mwingi wa kusoma,na hata hivyo si kwamba kukwepa kusoma tu hapana kama tukiangalia Tanzania yetu sasa ivi tunahitaji vitabu ambavo vitakuwa na muongozo wetu ,kwamba tunakitabu chetu cha kompyuta,vitabu ambavyo vinatakiwa vipatikane katika shule na hiyo ndo changamoto yetu kubwa ambayo ninaweza nikalia na serikali yetu,pili walimu wa tehama hawapewi kipaumbele kama walimu wengine"katibu wa shule hiyo Happyness Adolph Silayo akizingumza
Kwa upande
wao walimu wa Tehama wa shule ya secondary longido wameishukuru mamlaka ya
mawasiliano kwa kuadhimisha siku hiyo shuleni kwao na kuwapatia vifaa,pia
wameiomba serikali kuwatatulia changamoto kubwa walionayo hasa ya vitabu vya
kufundishia tehama na kujaribu kuomba mtiani ya tehama kutugwa.
Aitha bi
Annet ametoa rai kwa wadau
mbalimbali na serikali kujitolea vifaa
kama kompyuta na vitabu vinavyo kidhi mahitaji ya
wanafunzii
No comments:
Post a Comment