Katika
taarifa yake ya leo saa 11:15 jioni, TMA imetoa tahadhari kuwa, kuanzia
leo hadi keshokutwa kutakuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi
milimita 50 ndani ya saa 24 vinavyoambatana na upepo mkali unaozidi
kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili.
Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba. “Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika Bahari ya Hindi eneo la kisiwa cha Madagascar, hivyo kusababisha upepo mkali katika pwani ya Tanzania,” imesema taarifa hiyo.
TMA imewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki na kwamba, inaendelea kufuatilia hali hiyo na itatoa mrejesho kila itakapobidi.

No comments:
Post a Comment