Kiungo wa Manchester United Michael Carrick amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja. Carrick, mwenye Miaka 35, alitua Old Trafford kutoka Tottenham kwa dili ya paundi milioni 18.6 mwaka 2006 na kucheza mechi 458 akifunga bao 24.
Carrick, ambae Mkataba wake wa sasa ulikuwa ukiisha Juni 4, ameeleza kufurahishwa kuendela kuchezea klabu hiyo. Juni 4 inatarajiwa kuchezwa mechi maalum uwanjani Old Trafford kwa ajili ya kumuenzi Carrick kwa utumishi wake mwema na Man United.
Carrick, ambae ni mchezaji wa kimataifa wa England, akiwa na Man United ameweza kutwaa UEFA Champions Ligi, Ligi ya Ulaya, kombe la FA na kombe la ligi mara 2.

No comments:
Post a Comment