Raisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania ametengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa nishati na madini Proff. Sospeter Muhongo
Utenguzi huo umekuja mara baada ya kutolewa kwa ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini
Ripoti iliyowasililishwa ikulu leo, iliwasilishwa na kamati ya wataalam wa sekta ya madini kubaini aina na kiwango cha madini yaliyo ndani ya mchanga unaosafirishwa kwenda nje.
Katika makontena zaidi ya 200 yaliyokuwa yakichunguzwa, imebainika kuwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni moja za Tanzania.
Dkt Magufuli alivunja Bodi ya wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania TMAA na kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake kwa kushindwa kutimiza majukumu yake


No comments:
Post a Comment