LATEST NEWS

Sunday, May 28, 2017

Copa Del Rey: Messi, Neymar, Alcacer waipa kombe Barca


Barcelona wameifunga Alaves bao 3-1 kwenye fainali ya kombe la mfalme, Copa del Rey na kujipa ahueni baada wiki iliyopita kushindwa kuutetea ubingwa wao wa La Liga ulioenda kwa mahasimu wao Real Madrid.

Fainali hii ilichezwa huko Vicente Calderon Jijini Madrid na ndio mechi ya mwisho kabisa kwa kocha wa Barca Luis Enrique ambae anaondoka klabuni hapo.

Barca walitangulia kufunga dakika ya 30 kupitia Lionel Messi na Alaves kusawazisha kwa Frikiki ya Theo Hernandez Dakika ya 33. Barca walipiga bao 2 za chapchap dakika za 45 na 48 kupitia Neymar na Alcarer na kwenda Haftaimu 3-1 mbele.

Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Barca kutwaa Kombe hili.

No comments:

Post a Comment

Adbox