Kocha mkuu wa Sunderland David
Moyes amejiuzulu nafasi hiyo kufuatia timu hiyo aliyokuwa akifundisha
kushuka daraja kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza maarufu kama
EPL.
Moyes, mwenye umri wa miaka 54, alimfahamisha mwenyekiti Ellis Short juu ya kujiuzulu kwake kwenye mkutano uliofanyika jijini London Jumatatu.
Kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Everton na Manchester United alichukua nafasi ya Sam Allardyce kwenye klabu ya Sunderland, Julai mwaka uliopita, baada ya kocha huyo kupata kazi kwenye timu ya Taifa ya Uingereza.
Sunderland ilimaliza mkiani mwa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu, ikiwa na alama 24, baada ya kushinda mechi 6 tu.

No comments:
Post a Comment