Kati ya ligi zinazoonekana vitendo vya kibaguzi kutawala ni
ligi kuu nchini Italia almaarufu kama Serie A, wachezaji wengi sana
Wakiafrika wamekuwa wakikutana na vitendo hivi ambavyo sio vya
kiungwana.
Wikiendi hii ilikuwa zamu ya kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya
Ghana pamoja na klabu ya Ac Millan ambaye sasa anaichezea klabu ya
Pescara Sulley Muntari ambaye alikutana na mashabiki wakorofi wabaguzi
wa rangi.
Muntari anadai mashabiki wa klabu ya Cagliari ni kama walimpania
kwani tangu mchezo unaanza dakika ya kwanza walikuwa wakimzomea sana
kila anapokimbilia mpira huku wakiimba nyimbo za kuhusu ngozi yake.
Mbaya zaidi kwa Muntari anasema kulikuwa na kundi la watoto wadogo
kabisa ambao nao walikuwa na wazazi wao lakini cha ajabu watoto wale nao
walikuwa wakimzomea Muntari kutokana na rangi yake.
“Wakati kipindi cha kwanza tunacheza niliona kundi la watoto wakiwa
na wazazi wao wakiwa wananizomea sana, niliamua kuwafuata na kuwapa jezi
yangu kama mfano wakatulia” alisema Muntari.
Muntari anadai wakati wanarudi tena uwanjani kipindi cha pili
kulijitokeza kundi lingine ambao wao sasa walikuwa wakizomea zaidi na
kumuimba zaidi, kitendo ambacho kilimkera na kumuumiza sana.
“Wakati hili kundi lingine likinizomea nilijaribu kumfuata muamuzi
kumuambia kuhusu kelele hizo, cha ajabu aliniambia endelea kucheza mpira
badala ya kutuliza hali ya mashabiki, hapo nilikasirika sana na
nikaamua kuondoka”, Muntari alitoka dakika tank kabla ya mchezo huo
kuisha na kuifanya timu yake kumaliza 10 uwanjani.
Muntari amesisitiza kwa kuwaambia wazungu kwamba “hii ni rangi yangu
na najivunia” huku kocha wake Zdenek Zeman akimtupia lawama muamuzi wa
pambano hilo kwa kushindwa kutafuta namna ya kuwatuliza mashabiki.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus
Alessandro Del Piero amemkingia kifua Muntari kwa kusema kwamba wakati
mwingine ni vyema kufanya mambo ili kuwa onyo kwa mashabiki na waamuzi.
Monday, May 1, 2017
Home
/
MICHEZO
/
“hii ni rangi yangu na najivunia”Sulley Muntari awasisitizia wazungu wenye ubaguzi huko Italia
“hii ni rangi yangu na najivunia”Sulley Muntari awasisitizia wazungu wenye ubaguzi huko Italia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment