Siku moja baada ya tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
kufanyika na kutoa zawadi kwa wahusika, timu ya Simba ambayo ni mshindi
wa pili haikuwepo wala kutuma muhusika katika eneo la tukio ikihisiwa
kuwa ni muendelezo wa kugomea zawadi ya mshindi wa pili.
Jana ziliripotiwa habari za uongo katika mitandao ya kijamii kuwa
wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa Rais wao Evans Aveva wamekubali
nafasi ya mshindi wa pili na kufuta malalamiko yao FIFA kuhusiana na TFF
kuituhumu kutotenda haki.
Akikanusha habari hizo Makamu wa Rais wa klabu ya Simba, Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ amesema wao wapo nje ya mji wa Dar es Salaam kwa ajili
ya maandalizi ya fainali yao dhidi ya Mbao FC na si kweli kwamba
wamesusia tuzo.
Pamoja na hayo, Kaburu amesema timu yake imejiandaa vizuri katika
fainali hiyo ili waweze kuchukua ubingwa na kuweza kuwakalisha nchi
katika mashindano ya kimataifa.
Friday, May 26, 2017
Simba yakanusha habari za kusuia tuzo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment