LATEST NEWS

Friday, June 16, 2017

Ajali ya basi yaua watatu, 27 wajeruhiwa Haydom

picha kwa hisani ya millard ayo.com

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Haydom, kuelekea Mbulu Mjini, kuingia mtoni.

Ajali hiyo imetoka leo asubuhi, ambapo basi hilo limeingia kwenye mto ambao hauna maji uliopo kilomita chache kutoka mji mdogo wa Haydom. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema ajali hiyo ilihusisha basi la abiria la Kampuni ya Hamandos lililokuwa linatoka mji mdogo wa Haydom likielekea Mbulu Mjini.

 Mofuga amesema chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kukatika usukani (sterling road) na kukosa mwelekeo kisha kuingia mtoni na kugonga kingo za mto huo. Amewataja waliofariki dunia ni Gidaguy Samo (65) mkazi wa Kijiji cha Basodesh, Josephina Nade (45) mkazi wa Kijiji cha Gdihim na Neema Petro Amma (25) mkazi wa kijiji cha Haydarer wilayani Mbulu.

Mkuu huyo wa wilaya amesema miili ya marehemu Wamehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Haydom na majeruhi hao 24 wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo.

Amesema watu 27 walipokelewa kwenye hospitali hiyo, watatu walifariki dunia, kati ya 24 walio majeruhi, wawili bado hawajapata fahamu. “Majeruhi wanaoendelea kupata matibabu ni Sulemani Hussein, Samweli Zacharia, Katarina Daniel, Loth Baha, Captolina Lohay, Daniel Sanja, Felistiani Anthony na Dengu Matle,” amesema Amewataja majeruhi wengine ni Julieth Lowry, Grace Tumaini, Fanuel Thomas, Sabrina Thomas, Hagai Daniel, Edward Petro, na Olivery Fuumay. “Majeruhi wengine ni Gersael Akonaay, Sese Gwayadesh, na Daniel Gilengana” amesema Mofuga. Majeruhi wengine hawakuweza kufahamika mara moja majina yao.

No comments:

Post a Comment

Adbox