LATEST NEWS

Tuesday, June 27, 2017

Baba mzazi wa Mourinho azikwa mjini Setubal Ureno

TAZAMA PICHA 10: Kutoka kwenye mazishi ya baba yake Jose Mourinho
Jose Mourinho akiwa na baba yake mzazi enzi za uhai wake
Baba wa kocha mkuu wa Manchester United, Jose Mourinho, Jose Manuel Mourinho Felix amezikwa jana mjini Setubal Ureno. Mazishi hayo yamehudhuriwa na Jose Mourinho pamoja na familia yake.

Mzee Mourinho alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua muda mrefu. Alikuwa mwanasoka na aliwahi kucheza hadi timu ya taifa ya Ureno akiwa golikipa.

Jose Mourinho alitoa heshima za mwisho kwa mwili wa baba yake mzazi mzee Jose Manuel Mourinho Felix ambaye amefariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 79 baada ya miezi kadhaa ya kuugua.

Mourinho aliungana na mkewe Matilde, mtoto wake wa kiume Jose Jnr na Kocha msaidizi wa United Silvino Louro.




Jose Mourinho akisaidia kuweka bendera kwenye Jeneza lililohifadhi mwili wa baba yake

Meneja wa Manchester United akionekana mwenye huzuni wakati wa kuuaga mwili wa baba yake
Mourinho na waombolezaji wengine wakilibeba Jeneza la Felix kupeleka Kanisani 




Baba yake Mourinho alifariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 79 baada ya kuugua kwa miezi kadhaa


Mke wa Mourinho Matilde (kulia akivalia blauzi nyeupe) akimshuhudia Boss wa United akibeba Jeneza la baba yake


Jeneza lililobeba mwili wa Mourinho Felix likiwa ndani ya gari kabla ya kupelekwa Kanisani


Kocha wa timu ya kwanza ya Manchester United Silvino Louro (katikati) alikuwepo pia kumfariji Mourinho


Kundi la waombolezaji wakiwa nje ya Kanisa mjini Setubal kutoa heshima zao kwa mlinda mlango wa zamani Mourinho Felix

Binti wa Mourinho Matilde akionekana kufadhaishwa huku akimshikilia mama yake pamoja na kaka yake Jose Jnr



Kocha wa Makipa wa United Emilio Alvarez Blanco (katikati nyuma) na Aitor Karanka (kushoto nyuma) pia walikuwepo

No comments:

Post a Comment

Adbox