LATEST NEWS

Tuesday, July 11, 2017

Bocco na Wenzake wapya sita kikosini tayari kuivaa Rwanda.

                                                       
Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa stars imesafiri kuelekea mwanza kwa matayarisho kabambe huku kukiwa na wachezaji wapya kikosini kushiriki michezo yajayo.Kati ya hao ambao Kocha Mkuu Salum Mayanga amewaita, wamo wale aliowatangaza juma lililopita ambao ni John Bocco, Kevin Sabato pamoja na kinda Athanas Mdamu ambaye anacheza Alliance ya Mwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza. Katika kikosi chake kabla ya kuivaa Rwanda Jumamosi ijayo, wachezaji wengine ambao Kocha Mayanga amewatangaza leo ni pamoja na Kipa wa Serengeti Boys – timu ya taifa ya vijana ya Tanzania, Ramadhan Kabwili.
Taifa Stars inajiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 15, mwaka huu kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).

No comments:

Post a Comment

Adbox