LATEST NEWS

Thursday, July 13, 2017

BREAKING NEW;MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU YAWAACHIA HURU MASAMAKI NA WENZAKE WATANO


Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA,
Tiagi Masamaki (pichani kulia) na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa
na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh.
Bilioni 12.7.



Karama Kenyunko-Globu ya Jamii.

Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA,
Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya
uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7.

Washtakiwa
hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi baada ya upande wa
mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Timon
Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya
makosa ya jinai (CPA) kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi
ya washtakiwa hao.

"Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa
ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle
Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema
Wakili wa Serikali Timon Vitalis.
Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa.

Mbali
na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo iliyotokana
na sakata la makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA,
Habib Mponezya (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha,
Burton Mponezya (51).

Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa
Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31), Mchambuzi Mwandamizi wa
Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni za
Usalama na Ulinzi ICD, Raymond Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD,
Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28) wa kitengo cha Mawasiliano ya
Kompyuta ICT TRA.
Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa
watano tu ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya,
Burton Mponezya na Ashraf Khan.

Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni
Mpande na Khakis Ally Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa
mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa wapya, Khalid Yusuph Hassan na
Benson Vitalis Malembo.



----- ------ --------

No comments:

Post a Comment

Adbox