Wachezaji wa klabu ya Everton ya England wako jijini Dar es Salaam
nchini Tanzania kwa ziara yao ya kwanza kabisa Afrika Mashariki.
Wachezaji hao na wakufunzi pamoja na maofisa wengine wa timu
walipokelewa kwa mbwembwe baada ya kuwasili kutoka Liverpool. Ziara yao
ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu ya Premia, Uingereza.
Miongoni mwa wachezaji waliosafiri Tanzania ni Wayne Rooney ambaye
amerejea katika klabu baada kuwa Manchester United. Mashabiki wengi wa
soka wamefika Tanzania kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa
Kenya, Gor Mahia katika uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam
baadaye siku ya leo.

No comments:
Post a Comment