![]() |
| Diego Mardona akifunga bao lake maarufu hand of God dhidi ya Uingereza 1996 |
Diego Maradona ameunga mkono
utumiaji wa kanda za video licha ya kukiri kwamba bao lake la ''Hand of
God'' dhidi ya Uingereza 1986 halikufaa kukubalika.
''Kwa kweli mimi hukumbuka bao hilo kila mara ninapounga mkono utumizi wa teknolojia'' ,Maradona aliambia Fifa.com.
''Nilifikiria kuhusu bao hilo na kwa kweli bao hilo halikufaa kuidhinihswa''.
Maradona anasema kuwa alifaidika kutokana na ukosefu wa teknolojia katika kombe la dunia na haikuwa mara moja bali mara mbili.
''Nitakwambia kitu chengine -katika kombe la dunia la 1990 nilitumia mkono wangu kuondoa mpira uliokuwa karibu kuingia katika goli letu dhidi ya taifa la Usovieti.
''Tulikuwa na bahati kwa sababu refa hakuona.Hakukuwepo na teknolojia wakati huo lakini sasa ni mambo mengine''.


No comments:
Post a Comment