LATEST NEWS

Tuesday, August 1, 2017

David Rudisha ajiondoa mashindano ya London

Image result for David Rudisha
Bingwa wa dunia anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 David Rudisha amejiondoa kutoka mashindano ya riadha ya dunia yatakayoandaliwa karibuni jijini London kutokana na jeraha.
Raia huyo wa Kenya mwenye umri wa miaka 28, alisema katika ukurasa wake wa Twitter kwamba ni jambo la kuhuzunisha na kusikitisha kukosa kushiriki mashindano hayo yatakayofanyika Agosti 4 – 13.
Rudisha ni mwanariadha pekee kuwahi kukimbia china ya dakika moja sekunde 41 katika mbio hizo. Alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki jijini London mwaka 2012 na baadaye akashinda taji hilo katika mashindano yaliyoandaliwa Rio, Brazil mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment

Adbox