Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kupitia kamati yake ya utendaji ilikutana jana kujadili masuala kadhaa ikiwemo namna yakupatikana kwa mfumo madhubuti utakaotumika kuendesha ligi kuu ya Zanzibar. Hili linakuja baada ya mfumo uliopitishwa na klabu za kisiwani Pemba ambao uliwekwa baada ya Zanziabar kupatiwa uanachama wa kudumu CAF lakini kutokana na taarifa za kutolewa katika nafasi hiyo imeona umuhimu wa kukutana tena na wadau wa soka kutafuta njia mbadala.
Mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho msemaji wa ZFA, Ali Bakar amesema kamati imependekeza kukutana na klabu zote ili kupanga mfumo mpya utakaotumika kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Bakar ameongeza kuwa kamati hiyo pia imezungumzia uhamisho huku ikizitaka klabu kulipia ada ya uanachama kwa ramjisi, ada ya mwaka wilayani, sambamba na ada ya mashindano huku akisisitiza kuwa timu itakayoshindwa kufanya hayo haitashiriki msimu ujao.
No comments:
Post a Comment