
Tuzo hiyo hutolewa na jarida la soka la Ufaransa.
David de Gea, Philippe Coutinho na Sadio Mane, Kevin de Bruyne na N'Golo Kante, pia wameteuliwa.
Gareth Bale anayechezea Real Madrid hajajumuishwa kwenye orodha hiyo.
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi hata hivyo wapo.
Kane, 24, ameorodheshwa kushindania kwa mara ya kwanza baada ya kufunga mabao 43 katika mechi 37 akichezea klabu na taifa mwaka 2017.
Bale, 28, amefunga mabao matano pekee Real Madrid mwaka huu na ameonekana kutatizika tangu mwisho wa msimu uliopita.
Nyota wa Real Madrid Ronaldo, 32, alimpiku Messi na kushinda tuzo hiyo kwa mara ya nne mwaka jana.
Messi, 30, ameshinda tuzo hiyo mara tano, mara nyingi zaidi kuliko mchezaji mwingine yeyote duniani.
Aidha, ni Ronaldo na Messi ambao wamekuwa wakishinda tuzo hiyo tangu Kaka wa Brazil aliposhinda 2007.
Orodha kamili ya wanaoshindania Ballon d'Or
- Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund na Gabon),
- Karim Benzema (Real Madrid na Ufaransa)
- Leonardo Bonucci (AC Milan na Italia)
- Gianluigi Buffon (Juventus na Italia)
- Edinson Cavani (Paris St-Germain na Uruguay)
- Philippe Coutinho (Liverpool na Brazil)
- Kevin de Bruyne (Manchester City na Ubelgiji)
- David de Gea (Manchester United na Uhispania)
- Paulo Dybala (Juventus na Argentina)
- Edin Dzeko (Roma na Bosnia-Herzegovina)
- Radamel Falcao (Monaco na Colombia)
- Antoine Griezmann (Atletico Madrid na Ufaransa)
- Eden Hazard (Chelsea and Ubelgiji)
- Mats Hummels (Bayern Munich na Ujerumani)
- Isco (Real Madrid na Uhispania)
- Harry Kane (Tottenham na England)
- N'Golo Kante (Chelsea na Ufaransa)
- Toni Kroos (Real Madrid na Ujerumani)
- Robert Lewandowski (Bayern Munich na Poland)
- Sadio Mane (Liverpool na Senegal)
- Marcelo (Real Madrid na Brazil)
- Kylian Mbappe (Paris St-Germain na Ufaransa)
- Dries Mertens (Napoli na Belgium)
- Lionel Messi (Barcelona na Argentina)
- Luka Modric (Real Madrid na Croatia)
- Neymar (Paris St-Germain na Brazil)
- Jan Oblak (Atletico Madrid na Slovenia)
- Sergio Ramos (Real Madrid na Uhispania)
- Cristiano Ronaldo (Real Madrid na Ureno)
- Luis Suarez (Barcelona na Uruguay).
No comments:
Post a Comment