Na Fredy Jakuba KAHAMA
Maafisa ugani na maafisa kilimo wameagizwa kutokaa ofisini na kuhakikisha wanawajibika kuwasimamia wakulima kupanda zao la pamba kwa kufuata utaalamu ili kupata tija katika zao hilo.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Fadhili Nkurlu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema wakulima wanatakiwa kupanda kwa kutumia utaalamu watakaopewa na wataalamu wa kilimo na kuhakikisha kila mkulima analima zao hilo.
Aidha amewaagiza pia watumishi wa serikali kuhakikisha wanalima angalau ekari moja na kila mmoja asimamia shamba lake kikamilifu.
Kuhusu suala la pembejeo za kilimo Nkurlu amesema tayari wakulima wamekwishakopeshwa mbegu mpaka hivi sasa.
No comments:
Post a Comment