Wednesday, October 18, 2017

Vipigo vikubwa kuwahi kutolewa Champions League



Siku ya jana tulishuhudia kalbu ya Liverpool ikitoa dozi ya mabao 7 kwa 0 dhidi ya Maribor, hii ilikuwa kwa mara ya kwanza kwa Liverpool kufanya hivyo katika uwanja wa ugenini kwenye Champions League.

Mabao 7 sio jambo la kushtuka sana lakinj mabao 7 ugenini ilikuwa kipigo kikubwa sana, Liverpool wameshawahi kufunga mabao zaidi ya matano katika Champions League lakini haikuwa ugenini, kwa haraka haraka hivi ni vipigo vikubwa kuwahi kutolewa Champions League.

Arsenal 7 Slavia Prague 0, hii ilikuwa October mwaka 2007 katika uwanja wa Emirates ambapo Gunners waliwakaribisha Slavia Prague, mabao mawili kutoka kwa Theo Walcott, mawili kutoka kwa Fabregas na mengine kutoka kwa Hubacek,Hleb na Bendtner wakailaza Prague bao 7.

Bayern Munich 7 Shaktar Donestki 0, huu ulikuwa msimu wa mwaka 2014/2015 pale Allianz Arena, Thomas Muller alifunga mara mbili,Boateng, Ribery, Badstuber,Lewandoski na Gotzw waliongoza kikosi cha maangamizi kuwaua Shaktar.

Bayern Munich 7 Fc Basle 0, Bayern hawa hawa walikutana na Fc Basle mwaka 2012 na kuwapiga bao 7 kwa nunge, Arjen Robben alifunga mara mbili, Thomas Muller akafunga mara moja huku Mario Gomez akifunga mabal manne katika dimba la Allianz Arena.

Real Madrid 8 Malmo 0, hii ilikuwa mwaka 2015 palw Santiago Bernabeu ambapo Cristiano Ronaldo alifunga mara nne, Karim Benzema akafunga mara tatu huku Kovacic akifunga moja na kuwaua Malmo kwa jumla ya mabao 8 kwa nunge.

Liverpool 8 Bestikas 0, mwaka 2007 ambapo Liverpool ilikuwa kati ya timu za kuogopwa Ulaya, Bestikas walikwenda Anfield na mabao ya Yossi Benayoun aliyefunga hat trick, Peter Crouch mawili,Ryan Babel mawili na Steven Gerrad aliyefunga moja yaliwaaibisha Bestikas katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Adbox