
N Mwishehe, Globu ya Jamiia Said
Kwa
mujibu wa taarifa zinaeleza basi hilo limechomwa leo na wananchi wenye
hasira kali baada ya dereva wake kumgonga dereva wa bodaboda.
Akizungumza
na Michuzi Globu kwa njia ya simu muda huu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tanga Edward Bukombe amefafanua ni kweli amesikia taarifa za kuchomwa
moto basi hilo lakini halijachomwa mkoani Tanga kama inavyoelezwa na
baadhi ya watu.
Amesema baada ya kuona taarifa za kuchomwa basi
la Simba Coach waliamua kufuatilia lakini wamejiridhisha haikutokea
kwenye mkoa wao ila basi hilo limechomwa nchini Kenya.
Kamanda
Bukombe ameiambia Michuzi Globu kuwa basi hiyo ilikuwa inatoka Mombasa
nchini Kenya na taarifa walizonazo limechomwa huko huko nchini Kenya
kwani lilikuwa halijaingia kwenye mipaka ya nchi yetu ya Tanzania na
hasa mkoani Tanga.
Alipoulizwa iwapo anafahamu namba za basi
hilo linalodaiwa kuchomwa moto na dereva aliyekuwa analiendesha ,amejibu
wanaendelea kufuatilia kwa polisi wa nchini Kenya na kisha atatoa
taarifa kuufahamisha umma.
"Tunaendelea kukusanya taarifa na kwa
kuwa limechomwa huko Kenya tunawasiliana na polisi wa huko ili tuwe na
uhakika wa taarifa Kamili za tukio hilo.Hatujapata namba za
basi.Wananchi wasubiri tutaeleza kwa usahihi tutakapokamilisha kupata
ukweli zinazohusu tukio hilo, "amesema Kamanda Bukombe.
TAARIFA KUCHOMWA MOTO SIMBA MTOTO
Mapema
asubuhi ya leo katika mitandao ya kijamii zilianza kuzagaa picha
zinazoesha basi linaungua moto, na vyanzo vya moto huo ikawa inaelezwa
ni wananchi wenye hasira wamechoma moto basi la Simba Coach.
Taarifa
hizo zikawa zinadai tukio hilo limetokea Mkoa wa Tanga lakini haikuwa
inaonesha ni wananchi wa eneo gani walioamua kuchoma basi hilo.
Pia
taarifa hiyo imedai basi limochomwa moto kutokana na dereva wake
kugonga dereva wa pikipiki na hivyo wananchi wakaonesha hasira zao kwa
kulichoma moto basi hilo. 

No comments:
Post a Comment