Leo kunachezwa michezo mingi ya kirafiki lakini Ujerumani dhidi ya Hispania ni mchezo ambao hakuna mwanasoka popote duniani anaweza kuukosa mchezo huu, ni mechi kubwa sana na japo ni ya kirafiki ila imekaa kimashindano.
Kwa namna tu vikosi hivi vilivyofuzu kombe la dunia inaweza kukupa picha juu ya mchezo huu, vijana wa Joachim Lkw(Ujerumani) walishinda michezo yote 10 ya kufudhu huku Hispania wakishinda 9 na suluhu moja.
Ujerumani ni kikosi ambacho katika kizazi chetu kinatajwa kuwa kati ya vikosi bora sana kuwahi kutokea, kombe la shirikisho pale Urusi mwalimu Low alionesha hazina kubwa ya Wajerumani kuelekea kombe la dunia.
Mjadala kuhusu Hispania umekuwa tofauti sana kwani Hispania hii inaonekana tofauti na Hispania ile ya 2010, hawa Wahispania wa sasa wanaonekana wa kawaida sana na timu inaonekana kuanza kuchoka.
2010 Hispania walikutana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia na kama unakumbuka bao pekee la Carles Puyol liliizamisha Ujerumani wakaondoka katika michuano hiyo.
Timu hizi katika mechi walizokutana hakuna aliyeshinda sana japo Wajerumani wameshinda mara 9, Hispania wameshinda mara 7 ikiwa ni tofauti ya ushindi mara 2 huku timu hizo zikienda sare mara 6.
Upinzani zaidi wa timu hizi unaonesha kwani aliyevunja rekodi ya Hispania ya kufuzu kombe la dunia kwa ushindi 100%(2010) ni Ujerumani kwani mwaka huu wamefanya hicho walichofanya Hispania 2010.
Hadi sasa Ujerumani ndio wako nafasi ya kwanza ya viwango vya soka duniani, na hadi kufikia hii leo Ujerumani wamecheza michezo 21 bila kupoteza mchezo hata mmoja.
No comments:
Post a Comment