LATEST NEWS

Wednesday, April 18, 2018

Mamia ya watoto waliosajiliwa kupigana vita Sudan kusini waachiwa huru

Maelfu ya watoto wametumika kupigana vita vya kiaraia Sudan kusini

Zaidi ya watoto 200 ambao wameajiriwa kwenye makundi yenye silaha nchini Sudani kusini wameachiwa ukiwa ni mpango wa kuunga mkono shirika linalohudumia watoto, UNICEF. Baadhi yao walikuwa wapiganaji.

Katika sherehe iliyofanyika jimbo la Equatoria, wavulana 112 na wasichana 95 walikabidhi silaha, walipewa nguo za kiraia. Wanatarajiwa kupatiwa ushauri nasaha, kurudi shuleni na kupatiwa mafunzo ya kiufundi. Mwezi Februari watoto 300 waliachiwa huru.

Umoja wa Mataifa unasema kuna takriban watoto 19,000 ambao wanatumikia jeshi na wanamgambo nchini Sudani kusini.
Rais Salva Kiir na kiongozi wa kundi la waasi Riek Machar (kulia)

Watoto wakirejea nyumbani, wazazi wao watapatiwa msaada wa chakula kwa ajili ya kusaidia kupambana na upungufu wa chakula.Familia zinapokuwa na uchumi mbovu watoto hushawishika kujiunga na makundi ya watu wenye silaha.

''UNICEF, UNMISS na Serikali ambao ni washirika wamekuwa wakihangaika bila kuchoka kushawishi makundi yaliyo kwenye mgogoro ili waweze kuwaachia watoto '' alieleza Bwana Mahimbo Mdoe, mwakilishi wa UNICEF nchini Sudani Kusini''.


UNICEF South Sudan@unicefssudan

Children have the right to be #ChildrenNotSoldiers!
#UNICEF calls on all parties to the conflict in #SouthSudan to end the recruitment of children, and to release all children in their ranks. #ChildrenUnderAttack
5:45 PM - Apr 17, 2018
33
30 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @unicefssudan

Watoto hao walikuwa kwenye Jeshi la National Liberation Movement (SSNLM) ambalo mwaka 2016 walitia saini makubaliano ya amani na serikali.

Hivi sasa jitihada zinafanyika kuhakikisha watoto wengine wanaachiwa siku za usoni.
Sudan Kusini hali si shwari, njaa kali

Pamoja na jitihada zinazofanyika makundi hasimu yanashindwa kutii sheria za kimataifa kuhusu haki za watoto. Wakati mazungumzo ya amani yakirejea na mjadala kuhusu mustakabali wa serikali ya mpito, UNICEF imetoa wito kwa pande zote zinazohusika na mgogoro nchini humo kuacha kuwaajiri watoto kwenye vikosi vyao na kuwaachia waliopo kwenye vikosi hivyo.

Fedha inahitajika kuwezesha mpango huo wa UNICEF.

UNICEF nchini Sudani Kusini inahitaji dola za Marekani milioni 45 kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kuwaachia watoto kwenye vikosi na kuwakutanisha watoto 19,000 na familia zao miaka mitatu ijayo.

Sudani Kusini imekuwa kwenye mapigano kati ya makundi hasimu tangu mwaka 2013, miaka miwili baada ya kujitenga na Sudan.

No comments:

Post a Comment

Adbox