LATEST NEWS

Wednesday, May 17, 2017

Hospitali Marekani yafanikisha upasuaji mkubwa wanafunzi wa Lucky Vicent

Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji jana na sasa wapo wodini. Mbunge wa Singida Kaskazini,

Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao. Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.


Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.


 “Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema Amesema Doreen yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga, taya katika upasuaji uliochukua saa nne. Kesho Doreen atafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.

No comments:

Post a Comment

Adbox