
Katika ripoti yake ya jana,
kamishna huyo amesema, karibu wakimbizi elfu mbili na 750 wa Jamhuri ya
Afrika ya Kati wamemiminika katika mikoa ya Bas-Uele na Ubangi Kaskazini
(Nord-Ubangi), huko kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
![]() |
Wanawake na watoto wadogo ndio wahanga wakuu wa machafuko |
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wakimbizi hao
wamekimbia mapigano katika mji wa Bangassou wa kusini mashariki mwa
Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo na maeneo mengine ya mpakani.
Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa
Mataifa kuhusiana na masuala ya wakimbizi amesema, hali ya wakimbizi wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo si nzuri hata kidogo.
Hivi sasa baadhi ya wakimbizi hao wamepewa makazi katika maeneo ya mashuleni, kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Maelfu ya raia wamekimbia makazi yao kutokana na kuongezeka mapigano ya kutumia silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment