![]() |
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Abdolreza Rahmani-Fazli |
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi wa kuaminika wa
karibuni kabisa wa maoni, zaidi ya asilimia 72 ya watu waliotimiza
masharti ya kupiga kura watashiriki katika uchaguzi wa keshokutwa Ijumaa
hapa nchini, na kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka katika kipindi
cha siku hizi chache zilizobakia.
Uchaguzi wa 12 wa Rais wa Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran pamoja na uchaguzi wa tano wa mabaraza ya Kiislamu
ya miji na vijiji unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya Mei 19.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa
Iran, Abdolreza Rahmani-Fazli, alisema hayio jana usiku katika mahojiano
maalumu aliyofanyiwa na Kanali ya Pili ya Televisheni ya Shirika la
Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB na kuongeza
kwamba, watu milioni 56 na laki nne na elfu 10 na 234 wametimiza
masharti ya kupiga kura nchini Iran. Ameongeza kuwa, karibu maafisa
milioni moja na laki tano wanaendesha na kusimamia uchaguzi huo.

Amesema, kuna uwezekano mkubwa mshindi
wa uchaguzi wa rais akapatikana katika hatua ya kwanza ya uchaguzi huo
kutokana na baadhi ya wagombea kujitoa kwenye kinyangányiro hicho kwa
maslahi ya wagombea wengine.
Aidha amesema, matokeo ya uchaguzi
yatangazwa mara moja na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran, waziri wa mambo ya ndani ndiye mwenye haki ya
kutangaza matokeo ya mwisho ya kura naye atatangaza matokeo hayo mara
yatakapomfikia.
Pars Today
No comments:
Post a Comment