Bajeti ya Kenya ya mwaka 2017/2018, imesomwa jana kinyume na
inavyosomwa kawaida mwezi Juni, kutokana na uchaguzi mkuu utakaofanyika
Agosti mwaka huu, huku ikitangaza kusimamisha ajira katika sekta ya
umma.
Katika bajeti hiyo ya shilingi za Kenya trilioni 2.6 (Takriban
shilingi trilioni 52 za Tanzania) Waziri wa Fedha, wa nchi hiyo, Henry
Rotich ameondoa kodi kwenye mahindi yanayoagizwa kutoka nje kwa kipindi
cha miezi minne ijayo,
Aidha kodi imeondolewa kwenye dawa za kuulia wadudu za nchini humo pamoja na magari ya utalii yanayoundwa nchini Kenya.
Katika bajeti hiyo ambayo ni ya mwisho kwa serikali ya Jubilee
katika muhula wake wa kwanza, serikali imeongeza kodi kwenye kamari hadi
50% kutoka 7.5% ya awali kama njia ya kukomesha uchezaji kamari.
Serikali pia imetangaza kusimamisha ajira katika sekta za umma isipokuwa sekta ya elimu kama njia ya kupunguza matumizi.
Jumla ya Shilingi bilioni 524.6 za kenya katika bajeti hiyo zitatokana na mikopo kutoka nje na ndani ya nchi.
Shilingi bilioni 2 za Kenya zimetengwa kuwaajiri walimu, na
zingine bilioni 4 kuwalipia mtihani wanafunzi wa darasa la nane na
kidato cha nnemwaka 2017 na 2018 huku serikali za kaunti zikipata jumla
la shilingi bilioni 329.
Ili kuhakikisha kuwa vijana wana ajira, serikali imetenga shilingi
milioni 450 Ksh kwa kuboresha kiwanda cha Rivatex, na zingine milioni
250 kuboresha kiwanda cha maziwa cha New KCC.
No comments:
Post a Comment