Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
Afrika Masharika, Dkt. Suzan Kolimba alipokuwa Akizungumza na waandishi
wa habari.
Alisema kuwa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn imetokana
na mkutano kati yake na Rais Dkt. Magufuli uliofanyika baada ya mkutano
wa kawaida wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika
uliofanyika hivi karibuni huko nchini Ethiopia.
Alisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni pamoja na kukuza mahusiano
mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja na kujadili fursa
zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na
biashara.
“Mahusiano ya Tanzania na Ethiopia ni mazuri, Ethiopia imeonesha
nia ya kufungua Ubalozi wake hapa nchini hivi karibuni. Kwa sasa
Ethiopia inawakilishwa nchini na Balozi wake aliyepo Nairobi nchini
Kenya” alisema Naibu Waziri Kolimba.
Wakati wa ziara hiyo,Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn atakutana
na Rais Dkt. John Magufuli kwa mazungumzo, watashuhudia uwekwaji saini
wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza
na Waandishi wa Habari.
Aprili 01 mwaka huu, Waziri mkuu huyo wa Ethiopia atatembelea
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa Bandarini hapo, Dessalegn na ujumbe wake wataondoka siku
hiyo hiyo kurejea Ethiopia.
Hata hivyo, Mwaka 2015 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn
alitembelea Tanzania na kushiriki uzinduzi wa Kiwanda cha kutengeneza
dawa za kuua viluwi luwi vya mbu wanaoeneza Malaria kilichojengwa
Kibaha, Pwani kwa ufadhili wa Serikali ya Cuba
No comments:
Post a Comment