Monday, March 20, 2017

BASATA KUTOA TUZO KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SANAA







  Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa Akizungumza na Waandishi wa Habari        mapema leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Habari mkuu ,Agnes Kimwanga.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linataraji kuwazawadia wanafunzi Saba waliofanya vizuri katika sanaa za maonyesho na uchoraji katika shule tano za sekondari nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa amesema kuwa wameamua kutoa zaidi tuzo ili kuongeza hamasa katika masomo ya Sanaa katika shule za Sekondari.

“Tuzo hizi zitakuwa nyenzo kwa ajili ya kujenga
hamasa, ari, ubunifu na juhudi katika kuleta maendeleo kupitia masomo ya
sanaa. Katika program hii wanafunzi kutoka shule 5 za sekondari
zitakazohusika katika kupewa tuzo hizo, shule hizi ni Loyola, Azania za
Dar es Salaam, Bukoba ya Mkoa wa Kagera, Darajani toka Mkoa wa
Kilimanjaro na Arusha Sekondari toka mkoa wa Arusha.Amesema Shaluwa.

Amesema ni matarajio ya BASATA kuwa utoaji wa tuzo hizi utachochea wanafunzi
wengi kusoma masomo ya sanaa, kuongeza ubunifu katika kazi za Sanaa na kuwasaidia katika kuongeza ufaulu wao darasani hasa ikizingatiwa Sanaa ni nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.



 
 

No comments:

Post a Comment

Adbox