Monday, March 20, 2017

NMB Mobile TISS Kumaliza Tatizo la Foleni kwa Wateja



Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada,
Stephen Adili (wa kwanza kushoto) akizungumza na wanahabari kuzinduwa
huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS). Kulia ni Mkuu wa
Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage.[/caption]
NMB imezindua rasmi huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile
TISS), kutoka katika akaunti za benki hiyo, kwenda kwenye akaunti za
benki nyingine, sambamba na kufanya manunuzi na malipo.

NMB Mobile TISS, ni huduma ya kwanza kutolewa na benki nchini Tanzania,
ambayo imetajwa kuwa ni njia rahisi, salama na ya haraka katika mchakato
wa kutuma ama kuhamisha fedha kutoka NMB kwenda benki nyingine.

Akizungumza katika hafla ya kuitambulisha huduma hiyo kwa wanahabari, Kaimu       Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada, Stephen Adili
alisema NMB Mobile TISS ni mwarobaini wa wateja wao kutumia muda mrefu
kwenye foleni za kuhamisha ama kutembea na fedha mkononi. “Huduma hii
inakuja kumaliza tatizo la wateja kutumia muda mwingi kwenye mchakato wa
kuhamisha fedha. Muda ni mali na kwa kulitambua hilo, tumekuja na
huduma hii ambayo inafanyika popote, hata ukiwa ufukweni unapunga upepo.
Kaimu Meneja Mwandamizi wa Amana, Huduma za Bima na Huduma za Ziada,
Stephen Adili (mwenye suti ya bluu mbele) akizungumza na wanahabari
kuzinduwa huduma ya kuhamisha ama kutuma fedha (NMB Mobile TISS). Kulia
ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa NMB, Geofrey Mwijage.










        Aliongeza ya kwamba, NMB Mobile TISS haiishii tu katika kuhamisha fedha kutoka
akaunti ya NMB kwenda benki nyingine, bali inaenda mbali na kupokea ama
kutuma miamala ya mitandao ya simu za mkononi. Huduma hiyo inayoweza
kutumiwa na wateja wa NMB Mobile, inapatika na kwa mteja kubonyeza alama
nyota, kishanamba 150, alama ya nyota, kisha namba 66 na mwisho alama
ya reli na kufuata maelekezo (*150*66#).
 

Naye Geofrey Mwijage, ambaye ni Mkuu wa Uendeshaji wa Shughuli za Kibenki wa
NMB, lisema benki yake imejidhatiti vya kutosha katika kutanua huduma
miongoni mwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla. Alisema NMB Mobile
TISS inaenda kuwa mshirika sahihi wa Watanzania, katika kuharakisha
maendeleo yao na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
kuelekea Tanzania ya Viwanda. 


Source:MICHUZI

No comments:

Post a Comment

Adbox