Bunge la Somalia limeidhinisha orodha ya
baraza jipya la mawazari waliotangazwa na waziri mkuu wa Somalia Hassan
Ali Kheyre wiki iliyopita.
Katika kikao cha bunge kilichofanyika kuidhinisha baraza hilo,
kati ya wabunge 241, wabunge 224 walipiga kura za ndio, 15 za hapana, na
wengine wawili hawakupiga kura.Kheyre amesema serikali ya Somalia itachukua hatua haraka iwezekanavyo, ili kutatua changamoto zinazoikabili nchi hiyo. Mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri utafanyika wiki hii, ukifuatilia zaidi masuala ya usalama na ukame. Kheyre alitangaza orodha ya baraza jipya la mawaziri tarehe 21 mwezi huu, likiwa na mawaziri 41 na manaibu 26. Bw Gouled Hassan Dourad ameteuliwa kuwa naibu waziri mkuu wa Somalia. Bunge hilo la Somalia ndio pia liliomuidhinisha Hassan Ali Khaire kuwa Waziri Mkuu mpya.
Hatua hiyo inakamilisha awamu muhimu ya kisiasa Somalia baada ya Rais Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu kama Farmajo kuapishwa mwezi Februari baada ya kumshinda Rais wa zamani Hassan Sheikh Mohamud, ambaye uongozi wake ulikuwa ukikabiliwa na ukosoaji kutoka ndani na nje ya Somalia kwa masuala ya ufisadi. Farmajo naye pia alichaguliwa kuwa rais na bunge hilo hilo la Somalia. Baada ya kukamilika muundo wa serikali ya Somalia, nchi hiyo inatarajiwa sasa kuchukua hatua za kukabiliana na kundi la kigaidi la Al Shabab ili kurejesha uthabiti na usalama wa kudumu.
No comments:
Post a Comment