Thursday, March 30, 2017

Waziri Ummy Ashiriki Kikao Cha Wadau Wa Afya Afrika Mashariki

Nchi wanachama wa Umoja wa Afika mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki

Hayo yamesemwa jana na Waziri WA Afya,Maedeleo ya Jamiii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki kwenye kikao cha 14 nchini hapa

Waziri ummy alisema amefurahishwa sana na hatua iliyofikiwa na nchi wanachama wa Jumuiaya hiyo ambapo hivi sasa madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa

Katika hatua nyingine kikao hivho kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na
usimamizi wa pamoja wa waraalam wa afya,udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile Ebola,Mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na UKIMWI

No comments:

Post a Comment

Adbox